HIKI NDICHO SIMBA WANACHOKILILIA , AFE PUNDA MZIGO UFIKE>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Tuesday, November 28, 2017

HIKI NDICHO SIMBA WANACHOKILILIA , AFE PUNDA MZIGO UFIKE>>

Wanamsimbazi Lazima Sote Kwa Pomoja Tujue Timu Yetu Inataka Nini,Na Ni Lazima Tukubali Ukweli Pale Mtu Anapokuwa Mkweli Ktk Jambo Fulani.
Tusiwe Ni Wenye Kupinga Hata Kama Kuna Jambo La Kipuuzi Linafanywa Lakini Kwa Sababu Tuna Mapenzi Na Timu Ya Simba Basi Ujinga Wowote Unaofanyika Tuone Kuwa Ni Sawa Tu,Tuwe Na Upeo Wa Kuchambua Shaba Na Almasi...
Tumepewa Majina Mengi Na Tunapata Kashfa Nyingi Sana Kutokana Na Vitendo Vya Hawa Waliobahatika Kupata Nafasi Ya Uongozi Flani Ktk Timu,Hasa Pale Wanapopata Nafasi Za Kuongea.
Haji S.Manara Nampenda Sana,Hasa Pale Anapoona Kuna Baadhi Ya Mambo Hayaendi Sawa,Lakini Jana Nimesikia Kaongea Kitu Na Kuwakejeli Baadhi Ya Mashabiki Kuwa Ni Watu Wa Ajabu Na Hawajui Mpira Kisa Tumelalamikia Perfomance Mbovu Ya Timu Katika Mechi Ya Lipuli Na Simba.
Kiukweli Mechi Ile Simba Ilipata Nafasi Nyingi Sana Lakini Kutokana Na Kutokuwa Makini Kwa Forward Yetu Butu Kushindwa Kuzitumia Nafasi.
Sasa Kama Viongozi Wa Simba Ni kweli Wanamtuma Haji Manara Kuongea Utumbo Mbele Ya Tv Kila Mara Basi Hakika Nao Wanastahili Kupimwa Mkojo.
Simba Ina Ma Veterani Wengi Sana Ambao Wamecheza Mpira Ktk Timu Ya Simba Kwa Mafanikio Makubwa Sana,Na wengi Bado Wako Hapa Mjini Na Hawana Kazi Yeyote,Hawa Nadhani Kama Wangepata Nafasi Kama Hizi Huenda Ingekuwa Msaada Kwa Mashabiki Na Wachezaji Wenyewe Kwa Sababu Wasingeongea Utumbo Kila Wakati Na Wangeongea Kisoka Zaidi Na Wangekuwa Na Mchango Mkubwa Kwa Wachezaji Na Kuwapa Hamasa Ili Waweze Kufanya Vzuri Zaidi.
Haji Hajawahi Kucheza Mpira,Na Amekalia Malumbano Yasiyo Na Faida Yeyote Kwetu Zaidi Ya Kuitwa Majina Ya Ajabu Ajabu Tu Na Wapinzani Wetu.
Ifikie Mahali Ili Soka Letu Liende Mbele Basi Tuwe Na Watu Makini Ambao Mpira Uko Akilini Kwa Vitendo Na Sio Kuwa Baba Alikuwa Mchezaji.
Kwa Kweli Hizi Drama Za Kila Siku Zinachosha Sana Inabidi Simba Ibadilike Na Iache Kufanya Kazi Kwa Mazoea.
Nimesikia Akisema Eti Anaumia Sana Kwa Sababu Yeye Ndio Wa Kwanza Kuandamwa Pale Timu Inapofanya Vibaya,Yeye Ndio Wa Kwanza Kutukanwa Na Mengine Mengi Ya Kipuuzi,Baada Ya Kukasirika Nikacheka Sana.
Weka Kina Pawasa,Emanuel Gabriel Na Wengine Wengi Tu Waongee Habari Za Timu Kimpira Zaidi Sio Mashairi Tu.
Mimi Nasema Kweli Na Nitakuwa Mkweli Hata Kwa Mo Dewji Mwenyewe Pale Atakapoleta Habari Zisizoeleweka Buana.
Ifahamike Kuwa Simba Ni Kubwa Kuliko Yeyote Yule Na Ipo kitambo Na Itaendelea Kuwepo,Sasa Tuache Kujuana Sana Tufanya Kazi Kwa Maslahi Ya Timu Zaidi.
Viongozi Muwe Munaangalia Ya Kumtuma Huyo Bwama Kama Munahisi Ni Mtu Sahihi Kuendelea Kuwepo Hapo.
Ukitukana Nakutukana Bisha Kwa Hoja Twende Sawa.

No comments:

Post a Comment