GOLI LA KICHUYA LAWASAMBALATISHA KABISA MASHABIKI YANGA, WAANZA KUJITATHIMINI NINI WAFANYE, FUATILIA KUJUA - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Sunday, November 5, 2017

GOLI LA KICHUYA LAWASAMBALATISHA KABISA MASHABIKI YANGA, WAANZA KUJITATHIMINI NINI WAFANYE, FUATILIA KUJUA

Baada ya mechi ya Simba na Mbeya city nilifanikiwa kudaka baadhi ya mazungumzo ya wana yanga

Hasa kipindi cha pili,tulicheza nyuma ya mpira muda mwingi sana,striking yetu haikuwa ya kutisha km yao pengine wapinzani walikuwa bora,Singida wanafaa kupongezwa,wana timu nzuri na km wangecheza km jana game zote hakika wangekuwa on top of the race champion.

But all in all tuipongeze timu yetu! Tuliwakamata vizuri hasa dk 20 za mwanzo.Lakini pia tuwapongeze mabeki wetu kwa kuwa imara,ilibidi sometime Kelvin Yondani aongeze ukatili ili kukabiliana na Singida United ambao kupitia kwa Deus Kaseke walikuwa hatari kila wakikaribia langoni mwetu na hili lilijidhihiridha kupitia nyuso za Andrew Vincent"Dante" ambaye kuna wakati alionekana km anataka kutoka mchezoni lakini shukrani kwa Yondani,Kessy na Rostand ambao walimrudisha mchezoni kwa kumpa hamasiko.

Kikubwa ambacho nazidi kukiona ni timu yetu kutokuwa na kikosi kipana hasa majeruhi ya Thaban Scara Kamusoko,Amissi Tambwe,Donald Ndombo Ngoma na Juma Abdul aliyekuwa na kadi za njano jana na hivyo kukosa mtokea benchi ambaye angeenda kubadili sura ya mchezo-tuwaombee wapate nafuu haraka maana tunawamis sana.

Katika kiungo Papii Kabamba Tshishimbi bado   anaendelea kuwa mtu muhimu akisaidiwa na Raphael Daud na Pato Ngonyani ambaye jana alianza km holding midfielder huku wakikosa msaada wa Pius Buswita ambaye hakuwa akishuka sana ili kusaidia kuongeza watu km Godfrey Bahati Mwashiuya ambaye alikosa bao ambalo lingetufanya tutangulie.

Katika forward,Ibrahim Ajib Migomba na Obrey Cholla Chirwa walijahidi kadiri ya uwezo wao lakini walikosa penetration or through balls hali iliyopelekea kuna wakati Ibrahim Ajib kushuka hadi ktk 18 ya timu yake kuchukua mipira na kusaidia kuipandisha mbele.

Generally mchezo ulikuwa mzuri na mgumu wenye hadhi ya premier,ulikuwa mgumu kuliko mechi iliyopita dhidi ya Simba.

Kikubwa tunashukuru kwa moyo wa kujitoa,moyo wa uzalendo kwa timu uliyooneshwa na wachezaji wetu.Hakika walipambana na walikuwa tayari kuhatarisha maisha yao kwa faida ya timu.

Kwa sisi tuliokuwa tukiungalia mchezo ule kupitia AZAM TV,tuliona Singida wakipata faulo dk za majeruhi baada ya Kessy kuokoa hatari iliyoelekezwa langoni kwake na referee kuamuru kuwa ni faulo(hiyo si hoja yangu).Tuliona namna gani mzalendo mmoja alivyoshindwa kuficha mahaba yake kwa watoto wa Jangwani.
Huyo si mwingine bali ni Mbunge wa jimbo la Mtama-NAPE MOSES NNAUYE,camera za Azam zilimshuhudia jamaa akitetema miguuni kana kwamba anataka kuanguka-HAKIKA ALIKUWA KTK MBAYA YEYE PAMOJA NA WOTE WAITAKIAO MEMA YANGA MAANA ILIKUWA NI FAULO ILIYOKUJA KTK WAKATI WA HOVYO KABISA.

Mwisho,tuipongeze timu nzima,wachezaji na benchi la ufundi pamoja na sare tasa hakika walitutendea haki kwa upambanaji wao ndani ya uwanja-KONGOLE KWAO.

Ni maoni yangu.

No comments:

Post a Comment