STRAIKA wa kimataifa wa Yanga Mzimbabwe, Donald Ngoma, ni kama amelikoroga kwa uongozi wa timu hiyo, kutokana na kutimkia kwao bila ruhusa kutoka kwa waajiri wake hao.
Taarifa za uhakika ambazo zimenaswa na DIMBA, zinadai kwamba, Ngoma hayupo nchini, licha ya kwamba hakupata baraka kutoka kwa uongozi.
“Ukweli ni kwamba Ngoma hayupo hapa nchini, amekwenda kwao Zimbabwe, lakini jambo la kushangaza ni kwamba hajatoa taarifa kwa uongozi, yaani anashangaza sana huyu mchezaji,” alisema kigogo mmoja wa Yanga.
Taarifa hizo zililifanya DIMBA kubisha hodi kwa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwassa, ili kupata ufafanuzi, ambapo alisema hana taarifa zozote za kuondoka kwa Mzimbabwe huyo.
Alisema mchezaji huyo alifika ofisini hapo kuomba ruhusa, lakini kutokana na utendaji wa kazi wa klabu hiyo mchezaji huyo alitakiwa kupata kwanza ruhusu kutoka benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu George Lwandamina, ambaye naye angeuandikia uongozi barua kama angekubaliana na ombi lake.
“Hiyo ya kwamba yupo kwao sijui, ninachojua alikuja kwetu kuomba ruhusa tukamwambia aende kwanza akazungumze na benchi la ufundi ambao wangetujibu kwa barua, lakini mpaka muda huu hawajatujulisha kwa barua kama walimruhusu ama la,” alisema.
Mkwassa alisema endapo mchezaji huyo ameondoka bila ruhusa ya benchi la ufundi, ni suala la utovu wa nidhamu, ambao unapingwa katika klabu yao.
“Wakati anaomba ruhusa timu ilikuwa mkoani ikiwa inacheza na Kagera na Stand United, hivyo kocha hakuwapo, ikibainika ameondoka bila ruhusa uongozi utachukua hatua kali juu yake,” alisema Mkwassa.

No comments:
Post a Comment