Na Nesphory Buguja
Unaambiwa sare ya Lipuli FC dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa jana Jumamosi kwenye Uwanja wa Samora ni salaam kwa Yanga.
Mchezo huo ambao ulimalizika kwa wenyeji kutakata nyumbani na matokeo kwenda bao 1-1, na Simba kutamba kuwa ndiyo salaam nzuri kuelekea mechi ya watani wa jadi.
Mwenyekiti wa Tawi la Mpira Pesa Magomeni, Ostaz Juma, ameeleza kuwa sare hiyo inatoa nafasi kwa Simba kujipanga sasa kuelekea mechi hiyo inayoteka hisia za mashabiki itakayopigwa Aprili 29 2018.
Kwa mujibu wa Spoti Leo kupitia Radio One, Ostaz ameeleza kuwa Yanga kwa si timu yenye kuleta usumbufu bali watapata matokeo kutoka na sare ambayo imepatikana dhidi ya Lipuli.
Simba hivi sasa imefikisha jumla ya alama 59 kwenye ligi ikiwa imecheza jumla ya michezo 25 huku watani wake wa jadi, Yanga wakiwa na pointi 47 baada ya kucheza mechi 22.
No comments:
Post a Comment