STARS YASUKWA UPYA MANDAWA NDANI YA DIMBA ULIMWENGU MAJI YA SHINGO>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Monday, March 19, 2018

STARS YASUKWA UPYA MANDAWA NDANI YA DIMBA ULIMWENGU MAJI YA SHINGO>>

Mshambuliaji Mtanzania, Rashid Mandawa anayeichezea klabu ya BDF XI ya Botswana,ameongezwa kwenye orodha ya wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.

Stars inajiandaa kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Algeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Taifa Stars itaanza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Algeria Machi 22 2018, kabla ya kuikaribisha nyumbani timu ya taifa ya Kongo, Machi 27 2018.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga, awali aliita kikosi chenye jumla ya wachezaji 23 lakini baadhi wamepunguzwa kutokana na sababu mbalimbali.

Wachezaji walioitwa hapo mwanzo na sasa wameondolewa ni: Thomas Ulimwengu, Said Ndemla, Farid Mussa, Hamis Abdallah na John Bocco.

Walioongezwa na kufanya idadi ya wachezaji ndani ya kikosi hicho kuwa 21 ni: Himid Mao, Rashid Mandawa pamoja na  Shaaban Idd.

Kikosi hicho kitaondoka hapa nchini kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kirafiki utakaopigwa Mach 22 2018.



No comments:

Post a Comment