Kikosi cha Taifa Stars kinashuka Uwanjani'Mustapha Tchaker Stadium' kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Algeria jioni ya leo huko Blida, nchini humo.
Mchezo huo ambao ni wa kalenda ya FIFA, utakuwa unaipa nafasi Tanzania ya kulipiza kisasi baada ya kupoteza kwa mabao 7-0 wakati timu hizo zilipokutana mara ya mwisho 2015.
Tanzania ilifungwa idadi hiyo ya mabao wakati wa kuwania kufuzu kuelekea michuano ya Kombe la Dunia kuelekea Urusi mwaka huu.
Licha ya kufungwa, timu zote hazijafanikiwa kufuzu kushiriki michuano hiyo inayotarajia kuanza miezi kadhaa ijayo.
No comments:
Post a Comment