YANGA WAWATIA MOYO MASHABIKI KWA KAULI HII KUELEKEA MECHI YAO DHIDI YA RAHA FC>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Sunday, December 24, 2017

YANGA WAWATIA MOYO MASHABIKI KWA KAULI HII KUELEKEA MECHI YAO DHIDI YA RAHA FC>>

Baada ya Simba jana kuondolewa na kuvuliwa ubingwa wa michuano ya Kombe la FA,  kesho mabingwa wakwanza wa michuano hiyo Yanga itashuka dimbani kumenyana na timu ya daraja la pili Reha FC, mchezo ambao umepangwa kupigwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Mchezo huo ni muhimu kwa timu zote mbili hasa Yanga, ambao msimu uliopita walishindwa kulitetea taji hilo baada ya kipigo cha bao 1-0, kutoka kwa Mbao FC ya Mwanza.
Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na tahadhari kubwa kwani itakuwa ikicheza huku inakumbuka wakubwa wenzao Simba, walipopigwa mweleka na timu ya daraja la pili Green Worriors na kuvuliwa taji mapema huku watu wengi wakiwa hawaamini.
Kocha msaidizi Shedrack Nsajigwa, ambaye ndiye atakayekiongoza kikosi cha Yanga kesho, baada ya kocha mkuu kuchelewa kurudi mapumzikoni, ameahidi kupanga kikosi imara ili kupata ushindi wa mapema ambao utawaweka kwenye matumaini ya kusonga mbele hatua inayofuata.
Nsajigwa amesema lengo lao msimu huu ni kulirudisha taji hilo ndiyo maana wanaichukulia mechi hiyo kwa uzito mkubwa na kamwe hawatofanya masihara kwa kuwadharau wapinzani wao Reha FC.
"Hakuna timu ndogo tunachojua ni mchezo mgumu, ambao tunatakiwa kupambana ili kupata matokea hivyo tumejiandaa vyema kwa ajili ya mchezo huo na vijana wangu wote wapo sawa ikimtoa Thabani Kamusoko na Donald Ngoma ambao ni majeruhi," amesema Nsajigwa.
Kwaupande wake kocha wa Reha FC, ambaye aliwahi kuidakia timu hiyo miaka ya nyuma Ivo Mapunda, amesema anawaheshimu Yanga, kwasababu ni timu kubwa na nzuri lakini wamejiandaa kwa ajili ya kutoa upinzani kwa miamba hiyo ya soka Tanzania.
Kocha huyo amesema tim yake inaundwa na wachezaji wengi wadogo wasiokuwa na majina makubwa, lakini wanakwenda kupambana na Yanga bila hufu yoyote kwasababu mchezo wa mpira hauna rika.
"Nina wachezaji wawili watatu ambao ni wakongwe na wameshawahi kucheza timu za ligi kuu ambao ni Zuber Ubwa na Buju Selemani hivyo uwepo wao hao naamini utasaidia kuwaongoza vijana wengine kufanya vizuri kwenye mchezo huo,"amesema.

No comments:

Post a Comment