KUNA ushahidi uliowazi kabisa kuwa Asante Kwasi ni mchezaji halali wa timu ya Lipuli FC, na kwa klabu yoyote itakayomtumia nje ya waajiri wake wa sasa itakuwa ‘imepoteza’ mechi husika.
Mlinzi huyo wa kati raia wa Ghana ameteka vichwa vingi vya habari hasa baada ya kuhusishwa kujiunga na klabu ya Simba katika dirisha hili dogo. Kumekuwa na ‘mkanganyiko’ mkubwa kuhusu suala la Kwasi kujiunga Simba.
Jumapili iliyopita nilimsikia msemaji wa Lipuli, Clement Sanga akisema ‘wanamsubiri Kwasi mazoezini’ jambo ambalo limeongeza sintofahamu kwani tayari kuna picha zikimuonyesha mchezaji huyo akisaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao wa zamani wa Tanzania bara.
TFF inapaswa kusimamia haki katika hili
Kwassi amesajiliwa msimu huu na klabu ya Lipuli baada ya kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja na klabu ya Mbao FC. Alisaini mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo ya Iringa na hadi sasa ametumikia miezi minne tu, ikiwa na maana bado ana miezi nane katika mkataba wake wa sasa na Lipuli.
Kikanuni/kisheria mchezaji aliye na mkataba unaoanzia miezi sita huruhusiwa kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na klabu nyingine zinazomuhitaji. Kinyume na hapo ni makosa na klabu inayofanya mazungumzo ya moja kwa moja na mchezaji aliye katika mkataba mrefu na klabu nyingine inapaswa kuadhibiwa vikali.
Lipuli walitambua ‘njama’ ambazo Simba walikuwa wakizifanya kwa kuzungumza kisha kumlaghai mchezaji wao ambaye bado ana miezi nane katika mkataba wa sasa. Kwa kuwa TFF-Shirikisho la soka lipo, timu hiyo iliamua kuwataarifu wasimamizi na waendeshaji hao wa soka nchini kuhusu kinachofanywa na Simba dhidi ya mchezaji wao Kwasi.
Ajabu, licha ya kupewa taarifa rasmi kwa barua, TFF haikuwahi kuwaambia Simba kuhusu kosa wanalofanya kikanuni na kisheria na matokeo yake imefikia hatua ya Simba kumalizana na Kwasi kisha mchezaji huyo kusaini mkataba nao wakati wanatambua wazi mchezaji husika ni mwajiriwa aliye katika mkataba na klabu ya Lipuli.
Kwa sasa wakati ikifikiriwa ni hatua gani za kuchukuliwa, TFF haipaswi kuupitisha usajili huo na si hivyo tu katika hili Simba wanapaswa kupewa adhabu na adhabu stashili kwao ni kufungiwa kufanya usajili katika dirisha la usajili lijalo ili kujenga usawa.
Unakumbuka kuhusu suala la Pius Buswita na Simba ambalo ilipelekea TFF kumfungia mwaka mmoja mchezaji huyo wa Yanga? Naweza kusimama mahala na kusema nilisaidia sana kumrudisha Buswita uwanjani baada ya kuandika ‘madudu’ yaliyokuwa nyuma ya usajili wa mchezaji huyo kutoka Mbao FC hadi Simba.
Wakati ule nilishahuri TFF kuwapa adhabu pia Simba kwa maana walifanya kosa la kumsaini mchezaji ambaye bado alikuwa katika himaya ya Mbao. Kumfungia Buswita ilikuwa ‘dhaifu’ la kwanza ambalo lilianza kunipa picha kuhusu TFF ya Wallace Karia na Michael Wambura. Kama ni viongozi waliokuja kuinua mpira wa Tanzania naamini wanapaswa kuchukua hatua kali kwa kila klabu ambayo imekuwa ikiendeleza ‘umwinyi’ ambnao umekita mizizi katika soka la Tanzania.
Wakati ule alipoadhibiwa Buswita nilisema, TFF imekosea kwa maana Yanga ilimsaini kihalali mchezaji huyo mbele ya viongozi wake wa zamani (Mbao) na meneja wake. Wakati Simba wao walimlaghai Buswita na kumsaini kiholela. Makosa haya tukiyaendekeza kwa kuwa tu hufanywa na klabu kubwa nawaambia ukweli hatuwezi kupiga hatua yoyote katika soka japo unaweza kuona sura nyingi za wanasoka wa zamani pale TFF.
Kwasi ni ‘mswahili’ toka Ghana
Neno ‘Mswahili’ lina maana nyingi sana, mojawapo wa maana yake ni; mtu anayezungumza lugha ya Kiswahili, mtu mwenye maneno mengi, mlaghai, au mbabaishaji kiasi cha kutoaminika mbele yaw engine.
Kwasi alipatwa na msiba nyumbani kwao Ghana, hivyo aliomba ruhusa kwa waajiri wake Lipuli kwenda kumzika baba yake. Akiwa huko, tena siku chache tu zilizopita aliwapigia simu viongozi wake na kuwaambia amekwama kiasi katika mambo ya uchumi hivyo akaomba atumiwe nauli. Lipuli nawasifu sana. Licha ya kucheza madaraja ya chini kwa miaka 16 lakini wamerejea ligi kuu msimu huu wakiwa timu ya kisasa.
Japokuwa hawana wadhamini wengi, ila hao walionao sasa wamekuwa wakisaidiana kuendesha klabu kwa kulipa mishahara ya wachezaji kwa wakati, posho na kuimarisha kambi yao.
Baada ya Kwasi kuwaomba nauli, huku pia akiahidi kuwepo mazoezini Lipuli siku ya Desemba 16, uongozi wa klabu hiyo ulimtumia mchezaji huyo kiasi cha dola za kimarekani 670, pia waliamua kumtumia kabisa na mshahara wake wa mwezi Novemba hivyo kwa pamoja Kwasi alitumiwa dola zisizopungua 1000 na klabu yake wiki iliyopita.
Huku wakiwa hawajawahi hata mara moja kuzungumza na ungozi wa Simba kuhusu usajili wa Kwasi, Lipuli waliamini mchezaji huyo atakuwa mkweli na kujiunga na klabu yao wikendi iliyopita lakini badala yake zikavuja picha zikimunyesha mchezaji huyo akisaini mkataba wa kuichezea Simba!
‘Mlaghai’ huyu kwa hakika amewakosea sana Lipuli na watu wa Iringa kiujumla. Angeweza kuruhusiwa kuhama kama angetumia njia ya kiungwana, lakini matokeo yake amekuwa mtu mwenye tama huku akifanya makosa kwa kuamini klabu husika itayamaliza. TFF impe adhabu kali pia mchezaji huyu kwani taarifa zake walipewa kabla na waajiri wake.
Wanasheria waliosimamia usajili wake Lipuli washtakiwe
Siku hizi kumekuwa na wimbi la mameneja ambao katika soka la Tanzania watu hawa hujivika uwakala wa wachezaji. Kuna meneja/wakala wa Kwasi ambaye amekuwa akinukuliwa akisema Kwasi hana mkataba na Lipuli! Kwanza inashangaza, umeneja/uwakala wake ambao umeshindwa hata kumsafirisha mchezaji huyo kutoka Ghana hadi Tanzania na badala yake Lipuli ndiyo walisimamia hilo ili mteja wake awepo kazini kwa wakati husika.
Pili, katika soka la kulipwa hasa ngazi ya ligi kuu kama hii ya Tanzania Bara hakuna uwezekano wa mchezaji yeyote kucheza bila kuwa na mkataba unaotambulika TFF ambao utakuwepo pia katika TMS. Hivyo kusema Kwasi hakuwa na mkataba na Lipuli ni ujinga mkubwa katika kufikiri kwa maana mchezaji huyo asingeruhusiwa kucheza ligi.
Kwasi kama nilivyosema awali ni mchezaji halali wa Lipuli na bado ana mkataba wa miezi nane katika mkataba wake wa sasa na ameshalipwa mishahara miezi yote minne hivyo haidai kitu chochote Lipuli. TFF inafahamu vizuri na ukweli huu upo pamoja na ushahidi.
Lipuli na Simba hawajawahi kuzungumza kuhusu Kwasi zaidi ya Mnyate
Uhusiano wa kimazungumzo uliofanyika baina ya Lipuli na Simba katika dirisha hili la usajili ni kuhusu Jamal Mnyate. Lipuli iliwaomba Simba kwa maombi rasmi kupewa mshambulizi Mnyate kwa mkataba wa mkopo na hakukuwa na mazungumzo mengine yoyote yale. Licha ya kupewa Mnyate unajua kuwa Lipuli imetoa milioni kadhaa ili kumpata mchezaji huyo japokuwa ni usajii wa mkopo!
Sasa inakuwaje mchezaji wao aliye na mkataba wa miezi nane asajiliwe na timu nyingine bila ridhaa yao wala kupewa chochote? TFF isaidie haki ya klabu hii ndogo dhidi ya klabu kubwa na wachukue hatua za kinidhamu kwa wakosaji.

No comments:
Post a Comment