KUIKABILI CCM YA AWAMU YA TANO KWA KUSUSIA UCHAGUZI SIO JIBU SAHIHI JAPO NI JIBU.
Nikiwa mwanachama mtiifu na kiongozi ndani ya chama changu CHADEMA, nina imani kubwa na itikadi, falsafa na mlengo wa chama changu, huko sina wasiwasi. Nina iamini katiba ya chama changu inayonitaka niheshimu maamuzi ya vikao vya chama na nayaheshimu, hapa nachotaka kuonyesha ni dukuduku langu juu ya uamuzi uliofikiwa na kamati kuu ya kwamba kama maswala flani hayatafanyika basi hatutaingia kwenye uchaguzi mdogo wa hizi kata 6 na majimbo 3 likiwemo lililokuwa la Mh. Lazaro nyarandu. Nimeumizwa na haya maamuzi ambayo pia yameungwa mkono na vyama vyote vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA.
Naamini kamati kuu inayo think tank kubwa, ukawa kwa ujumla wanayo think tank kubwa pia, so naamini maamuzi yamefanyika kisayansi na kitaalamu zaidi na kwa kutumia uzoefu wa hali ya juu sana, sina wasiwasi na hilo, ila nachukulia kama mimi Dan ningekuwa na nafasi ya kushauri ningesema nini???
Binafsi nisingeshauri kususia uchaguzi, niliamini njia sahihi ni kuingia katika uchaguzi kulingana na hali jinsi ilivo, hatutaipata tume huru kwa kususia uchaguzi, tume iliyopo haiko tayari kukaa na vyama vya upinzani kama wadau wa uchaguzi, serikali iliyopo madarakani inatamani upinzani ufe ibaki CCM peke yake. Katika mazingira kama haya kutegemea negotiation ifanyike sio sahihi.
CCM wako tayari kuua CHADEMA hatuko tayari. Kwangu hii ni dhana potofu kabisa kuiamini. Nasema kama hauko tayari kuua hauko tayari kutawala pia. Kuua sio mpaka utumie risasi, au mapanga au sumu. Unapoingia kwenye uchaguzi lolote laweza kutokea, ukimshinda unayegombea nae ANAWEZA KUPANDWA NA PRESHA AKAFA KWA PRESHA, asa huwezi kusema kwa kuwa uliyemshinda amekufa basi unajiuzuru, yeye anakufa unaendelea kutawawala au kuongoza, asa kutanguliza woga wa kufa au kumwaga au kushuhudia damu ni uwoga wa kuyakabili mapambano. kuna kina mwangosi, kina mawzo, damu zao zimemwagika, Ben hatujui hatima yake. hizo pia ni damu zilizotangulia hatuwezi kuuaminisha umma kwamba hizo ndio damu zilizostahili kumwagika na sio zetu, THE ONLY THING YOU CAN OFFER IN A REVOLUTIONARY STRUGGLE IS YOUR BLOOD AND NOTHING MORE.
CHADEMA inapaswa kuingia kwenye mapambano na ccm kwa kuchungulia kwanza ccm wamekuja na maandalizi gani. Wakicheza fair, tuingie fairly, wakicheza rafu ccm, na chadema tucheze rafu, wakiingia na mawe ccm, na chadema tuingie na mawe, wakiingia na mapanga na sisi tuingie na mapanga. Na kwa kuwa tume hairuhusu mazingira haya kikubwa ni kuyaacha yatumike pande zote au sote tusimamishe mchezo, tuamue kuwa fair. LAKINI MMOJA KUINGIA NA PANGA UWANJANI SISI TUKAONDOKA UWANJANI, NI MBINU DHAIFU.
Naangalia kwenye kadi yangu ya CHADEMA wajibu wangu namba tano kama mwanachama ni KUWA TAYARI KUPAMBANA NA NAMNA YOYOTE YA UONEVU, UKANDAMIZAJI, UDHALILISHAJI NA UBAGUZI. Asa najiuliza napambana na haya mambo kwa njia ipi kama hali iko hivi? Kwa kususia uchaguzi waonevu wakatamba? Hapana, hapana tena hapana.
Nimechukulia mfano wa mbakaji, unapokuta mwanamke unayempenda naye anakupenda anabakwa na jitu kama JOHN CENA au yeyote akiwa na siraha, bado Yule mwanamke anakupigia kelele umwokoe na Yule mbakaji huku akijua huna nguvu kama yeye na hata siraha huna ila akikazana kukuita umwokoe, unawezaje kumwacha abakwe kwa kisingizio Yule ana panga, kisu, bunduki au siraha yoyote? Hauna budi kujitosa kupambana kufa kumwokoa mpenzi wako kwenye mikono ya mbakaji, yawezekana katika kupambana ukafa wewe, mwanamke au mbakaji lakini yote yatakuwa matokeo yako wewe kumuonyesha mpenzi wako kwamba nguvu uliyonayo sio siraha bali mapenzi kwake yanatosha kumfia, maana hata yeye anapokataa kubakwa ni kwa sababu ya mapenzi yake kwako. Akiona huna mpango wa kumfia ANAWEZA KUAMUA KUMKUBALIA MBAKAJI AMBAKE KIRAHISI NA HATA AMKUBALIE MAPENZI MAANA KUKUPENDA WEWE HAKUNA MSAADA TENA KATIKA KIPINDI AMBACHO YEYE AMEPASWA KUFANYA MAAMUZI YA NANI AMTUMIE. Hivi ndivo wanachama wetu watakavovunjwa moyo tukiacha ccm iwabake.
Nasema hivo maana chama kisichopendwa kinapolazimisha kutawala watu wasiokipenda ni DHAHIRI KINAWABAKA MAANA HAWANA MAPENZI NACHO, kukaa kukilaumu hicho chama, au kukiita mje kujadiliana sio njia sahihi zaidi ya kukikabili kukiua au kukiumiza kukidhi shauku ya huyu anayetaka umtawale au umwongoze wewe. Hakuna namna na hakuna sababu ya kukaa na ccm mezani zaidi ya kukutana nao field katika giza au katika nuru, vyovyote ili mradi tuhakikishe wananchi wanapata nafasi ya kuchagua itikadi wanayoitaka au kufuta vyama vingi. Lakini kumwambia mbakaji kwamba kama hutaweka siraha chini mi sipambani na wewe, wakati unajua njia pekeee aliyonayo ni kubaka maana hapendwi!!!! Ni kumwambia mpenzi wako kwamba huna sifa ya kuwa kama anavokuchukulia.
Nachukulia jimbo la lazaro nyarandu, wakati anajiuzuru ubunge alisema wananchi wachague itikadi wanayoitaka, akimaanisha watu wake wako tayari kumchagua tena akitokea kwenye itikadi nyingine. Hakuuacha ubunge jumla, aliacha ubunge wa ccm, leo tunapoenda kuwaacha wana singida kaskazini waongozwe na ccm tena ipite bila kupingwa, kweli tumewatendea haki wana singida kaskazini kuchagua itikadi wanayoitaka? Je tumemtendea haki nyarandu na kuonyesha kwamba uamuzi wake ulikuwa sahihi? Je wengine ambao wangetamani kuhamia upinzani ili wagombee upya tunawapa somo gani? BORA TUNGEACHA SEHEMU ZOTE TUKASIMAMISHA WAtGOMBEA KWA NYARANDU NA JIMBO LA LONGIDO.
Nachoamini ni lazima kubadili mbinu zilizotumika kuikabili ccm kipindi kile na ccm ya leo isiyoamini katika kufanya negotiation, ccm isiyoheshimu kuomba ridhaa kuongoza bali kulazimisha mapenzi hata isipokubalika lazima uikabili kwa njia tofauti. Sio lazima tushinde hizo kata zote na majimbo yote, LAKINI KUSHIRIKI UCHAGUZI NI JUKUMU LETU NAMBA MOJA. Kuna haja gani ya kuhimiza ujenzi wa misingi tukajaza takwimu za wanachama wakajaa moyo na mapenzi kwa chama, tukawapa matumaini ya kuiongoza dola afu ccm wakishika mapanga na kukata watu wanne au watano tunajitoa kwenye uchaguzi? Next time tunasusia uchaguzi? Hapo inabidi tufikirie upya, wakati tunahimiza watu kujiunga na chama chetu wanashawishika na sera zetu, itikadi na falsafa na malengo wanajua tuna ubavu wa kuyakabili haya YOTE, kuyasusia ni mbinu dhaifu kuliko zote ambayo sitakuja kukubaliana nayo hata siku moja.
Kususia uchaguzi kungefaa kwenye nchi kama sweeden, USA, UK, nk ambako demokrasia iko kiwango cha juu sana lakini sio kwa Tanzania hii ya sasa ambayo ADUI NAMBA MOJA WA AWAMU YA TANO NI DEMOKRASIA. Nimeangalia sehemu nyingi ambazo watu wamesusia uchaguzi hakujawahi kuwa na matokeo ya maana zaidi ya kuwavunja mioyo wafuasi. Nimeangalia Zanzibar, hata kama CUF wasingeshinda, kushiriki uchaguzi ilikuwa muhimu ili kuwe na wawakilishi kwenye bunge la jamhuri na baraza la wawakilishi pengine hata kupata makamu wa kwanza wa rais. Leo hii tumesusa, wao wamekula na ZECHA baadae akapewa tuzo, hivohivo ccm wameendelea kuongoza hata kama watu hawataki lakini wamefika mahali wanazoe sasa kuongozwa na wasiyempenda, TUNAWAFANYA WATU WAANZE KUUZOE UDIKTETA TARATIBU kwa kususia kwetu.
Nakumbuka mchakato wa katiba mpya haukuja kwa sababu KIKWETE aliichoka hii ya 1977, bali maandamano yaliyoongozwa na Dr. slaa na viongozi wengine nchi nzima na yale ya 05/01/2011 Arusha, yalimsukuma JK aseme nitaiachia Tanzania katiba mpya. Hayo yalikuwa matunda ya nguvu ya umma. SASA MKT WANGU NAULIZA NI LINI UTATUTANGAZIA KU APPLY NGUVU YA UMMA ZAIDI YA HIKI KIPINDI CHA UCHAGUZI NA KUDAI TUME HURU YA UCHAGUZI?
Naangalia watu wa karibu na ccm, ni serikali ya Kigali, M7, Chama cha kikomunisti cha CHINA, ZANU PF ya mgabe na vingine. Hivi kati ya hawa kuna wa kuishauri ccm ikae meza moja na wapinzani kujadili umoja wa kitaifa? Kagame? M7? Au rais wa china ndo aishauri ccm kupata maridhiano ya kitaifa? Wao umoja wa kitaifa sio ishu, lao ni kutawala. Mfano china ukikutwa unasoma gazeti tu linalomuongelea vizuri Dalai Lama unaweza fungwa maisha, na hakuna siku Dalai Lama ataruhusiwa arudi China. Hivohivo sahivi na sisi tunalazimishwa kusoma uhuru na jamvi la habari sio Tanzania Daima, Raia Mwema, Mawio wala, Mwana halisi. Afu tunategemea kukaa na hawa watu meza moja?
Mkt wangu Mbowe chama chetu kina redbrigade waliopikwa kabisa kulinda mali za chama na viongozi, hii nchi ina kata zaidi ya 20,000. Hivi ungeagiza kila kata ilete red brigade wawili tu kwenda kwenye maeneo ya uchaguzi kulinda mali za chama, wapiga kura wetu na viongozi wetu kuna ambaye angepata ujasiri wa kushika panga kutujeruhi kweli? Siamini km ingewezekana hata siku moja. Naangalia njia anayoitumia Bob wine kumkabili m7 mpaka nakuwa na wivu.
Agiza madiwani wote, wabunge wote, viongozi wa bavicha wilaya na mkoa mkt na katibu, tufurike kuhakikisha wananchi wanapewa haki ya kuchagua kiongozi wanayemtaka. Sio kuandika barua au waraka wa siri, tutangazie wazi na dunia ijue tumeenda kuitafuta haki ya kuchagua na kuilinda, huo ndo utakuwa mwanzo wa kuipata tume huru ya uchaguzi, nakuhakikishia nitakuwa wa kwanza kuitikia.
CCM hawako tayari kuachia uongozi kupitia sanduku la kura, kama wako tayari kumwaga damu ni hiyo damu itawafanya waachie nchi. nje ya hapo tutasusia uchaguzi hata 2019, 2020 maana tume itakuwa ileile, ambayo MKTwake anateuliwa na MKT wa ccm.
KAMATI KUU INA WATU MASHUHURI, WASOMI WABOBEZI, WA KWELI, WAZALENDO WENYE KILA SIFA YA KUFANYA MAAMUZI TUKAITIKIA AMINA HATA BILA KUKOOA. LAKINI YAWEZEKANA NI WAKATI WA MUNGU KUMTUMIA DAUDI KUMUUA GOLIATI AKAWAACHA MAJEMEDARI NA NYOTA ZAO.
Mzalendo wa nchi yangu kutoa Kasulu

No comments:
Post a Comment