WACHAMBUZI WAILILIA ARSENAL BAADA KUILAZA TOTTENHAM - KASULUWADAU.COM - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Monday, November 20, 2017

WACHAMBUZI WAILILIA ARSENAL BAADA KUILAZA TOTTENHAM - KASULUWADAU.COM

*DABI YA LONDON KASKAZINI*

Katika ulimwengu wa soka week hii  ilitawaliwa na kile kinachofahamika na wapenz wa soka la ulaya kama dabi ya kaskazini mwa london kwa kifupi NLD  japo kwa sie wanasiasa tukiona neno NLD kwa haraka tunakikumbuka chama cha marehemu mzee Emanuel Makaidi ambacho kinaitwa National League for Democracy kifupi NLD, licha ya ukongwe wa usajili wake nchini lkn pamoja na kupenda kwangu siasa lkn marehemu ni mtu pekee ninayemfahamu ktk chama hicho. Wana ndoto za kuchukua dola? Mie sijui nawaachia wao, leo niko na NLD ya ulaya yaani North London Derby. Dabi hii inavihusu vilabu viwili vya Arsenal na Spurs.

Ktk wiki ya mjadala kuhusu Dabi hii mara unaibuka mjadala unaoushika dunia pale maeneo ya Rhodesia ya kusini kama ambavyo ilifahamika miaka ya nyuma, kama sijasahau miaka hyo ilikuwa chini ya mtu aliyejiita cecil Rhodes, mzungu huyu aliyekuwa kiongozi wa kampuni lililoitwa British South African Company ktk kipindi cha utawala wa makampuni maarufu kama company rule in Africa. Huku Rhodesia zinaibuka habar za kupinduliwa rafiki wa  Wenger, ndio ni rafiki kwa sabb wana sifa zenye kufanana kwa sehemu kubwa mno.

Kwanza wote ni wasomi wazur wa elimu dunia kama wanavyoita vijana wa kileo, mmoja akiwa profesa wa uchumi lkn mwingine akiwa na degree zaid ya 7 za kusomea tu, ila wawili hawa wana sifa ya kuongoza kwa muda mrefu zaid ktk maeneo yao na kutokuwa tayar kuacha nafas zao licha ya kelele nying kutoka pande mbali mbali za dunia.
Naam, huyu mmoja ni comrade  hasa maana aliingia msituni na kupambana kuiongoza Rhodesia. Asili ya wao kule ni mapambano mno, nakumbuka ile Chimurenga War au kama wazungu walivyoiita Shona and Ndembele Resistance kipindi washona na wandembele walivyoungana kupigana dhid ya dhuluma za mabeberu weupe. Mengi siyakumbuk kwa sabb nilikuwa mdogo sana mwaka 1884 ila nakumbuka palichafukwa mno.

Baada ya jeshi kuonekana mtaani kisha baadae chama kikongwe kabisa Africa cha ZANU PF kukaa na kutangaza kumng'oa comrade Mugabe jion Comrade akalihutubia taifa runingani lkn dunia nzima ikiwa imejiandaa kusikia akitangaza kujiuzulu hotuba yake ikajaa mipango kabambe ya zimbabwe mpya. Akamaliza kwa kutangaza kuongoza kikao cha chama ambacho kilitangaza kumfukuza. Kwa mbali nikakumbuka kipindi Wenger watu wakipiga kelele aondoke pale Arsenal, na baada ya kumaliza msimu vibaya mno watu walijua utakuwa mwisho wa Wenger lkn aliongeza mkataba kwa mbwembwe na kutoa hotuba alioashiria bado yupo yupo sana.
Naam hawa ma comrade hawataki kung'atuka wapo na bado wapo wapo sana.
What do they have in common? Ni ngumu mno kuwang'oa.

Turejee kwenye Dabj yenyewe ya kaskazini, hii nayo ilitawaliwa na mijadala ambayo wao waliita power shift kutoka Arsenal na kuhamia Spurs, wachambuzi wengi walionekana kuamini kuwa power ime shift, sijajua kwa vigezo gani au ni kwa spurs kumaliza juu ya Arsenal kwa msimu mmoja tu licha ya Spurs kumaliza bila trophy na Arsenal kumaliza na trophy moja. Vivyo hvyo kule Rhodesia kinachogombewa ni power tu, sio kwa comrade ila kwa wale wanaoonekana ni warithi wake, wanaotishia kumng'oa comrade ni kwa sabb comrade anaonekana kulalia upande wa mmoja wanaogombea kumrithi lkn mrithi huyo hakuteseka kuikomboa Rhodesia masikini na wale ma comrade wengine waliopambana wanaona si sawa, haiwezekani ambaye hakuteseka vitan aje ale keki kiulaini kwa sabb tu eti ni baby wa comrade, hawa jamaa ndo kitu hawataki kusikia. Kilichotokea kule landan ya kaskazini baada ya mchezo na kinachoendelea kuonekana pale Rhodesia ni kama vile ni ngumu mno ku shift power. Kule landan Spurs alikandwa za kutosha na pale Rhodesia mzee aligonga speech ya mbwembwe mno na kumalizia kwa kupigiwa salute na wakubwa wote wa jeshi. Bado anayo power.

Mchezo wenyewe,
Spurs alizidiwa karibu maeneo mengi ya uwanja, licha ya kuonekana kuwa na possession kubwa lkn hakuwa tishio sana, mzee wenger ni kama huwa anabeti, kwa sabb kumuanzisha sanchez lacazette na ozil pamoja ni jambo ambalo kila kocha angekuwa akifanya hasa ktk game kubwa kama ya spurs ambayo unahitaji matokeo, lkn utashangaa game nying hawaanzi pamoja lkn walipoanza pamoja mabeki pinzani walijuta kwa nn wamekutana nao. Hawa watu walikuwa threat muda wote, pale kati xhaka akicheza na Ramsey walikuwa aggresive sana, na hapa ndipo walipoanza kuwapoteza spurs, huko nyuma mustafi na kos6 walicheza vyema na kuwafanya wakina Kane waonekane wazururaji tu uwanjani. Yapo mengi ya kueleza ktk mechi hii ila nimechoka kuandika,

Mwisho, yule ozil amekuwa kama haruna niyonzima wa yanga, haruna alipokuwa akitaka mkataba mpya pale jangwani utajuata kukutana naye, jamaa alikuwa anacheza uwanja mzima, anakaba na anapiga pasi za maana na kuifanya team nzima icheze, vile ozil alikuwa akipiga pasi af aki track back kama wanavyosema kwa lugha ya malkia ilikuwa jambo la kushangaza na kufurahisha mno, akatengeneza nafasi 4 na assist moja Arsenal ikiua, ktk mazingira kama haya Spurs ilikuwa lazima afe tu.

Anyway ujinga wangu niachieni mwenye maana hata sikumbuki nilichoanza kuandika ila nakumbuka hapa ninapomalizia.

Karibu .

No comments:

Post a Comment