Ukiachana na Mzee Akilimali anasubiriwa kwa hamu ili atimuliwe kwenye mkutano na wanachama wa Yanga, anayesubiriwa kupokewa kwa hamu ni Yusuf Manji.
Wanachama wa Yanga wanamsubiri Manji kwa hamu kubwa ambaye amealikwa katika mkutano huo.
Manji aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Yanga, atakwenda katika mkutano huo kama mwalikwa.
Kuna taarifa ameshawasili, lakini hazijathibitishwa. Mkutano wa wanachama wa Yanga unafanyika Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo.
“Tumeambiwa yuko kwenye ofisi kule, sasa tunasubiri tuone kama ni kweli,” alisema mwanachama mmoja akiwa na wenzake waliokuwa na shauku ya kumuona Manji.
No comments:
Post a Comment