SIMBA WAMTIMUA MWAJALI KWA SABABU HIZI , SOMA HABARI KAMILI HAPA>>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Monday, December 11, 2017

SIMBA WAMTIMUA MWAJALI KWA SABABU HIZI , SOMA HABARI KAMILI HAPA>>>

HATIMAYE Wekundu wa Msimbazi Simba, wamemtupia virago nahodha wao Method Mwanjali raia wa Zimbabwe.

Uongozi wa Simba umefikia hatua ya kuachana na nyota huyo kutokana na umri wake kuwa mkubwa hivyo kukinzana na falsafa ya klabu hiyo kongwe inayosifika kwa kuibua makinda wengi wenye vipaji.

Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya klabu hiyo tayari wamemalizana na nyota huyo, aliyejiunga na Wekundu hao Julai mwaka jana akitokea kikosi cha Caps United ya nchini Zimbabwe akisaini mkataba wa miaka miwili.



Chanzo cha kuaminika ambacho hakikutaka jina lake kuwekwa wazi, kilisema kuwa, “Tumeamua kuvunja mkataba na Mwanjali kutokana na mapendekezo ya kocha wetu Joseph Omog, ambaye aliomba aachwe na kutafuta mchezaji mwingine ambaye ni kijana, umri wa Mwanjali ni mkubwa sana na kwa sasa hivi hata kiwango chake sio kama kile ambacho alikuwa nacho wakati anakuja,”.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa kamati ya usajili iko katika mchakato wa kuhakikisha mbadala wake anapatikana kabla ya dirisha la usajili kufungwa Disemba 15 (Ijumaa ya wiki hii).

No comments:

Post a Comment