SIMBA SASA BALAAA , WAPITISHA FAGIO KWA VIGOGO>>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Monday, December 4, 2017

SIMBA SASA BALAAA , WAPITISHA FAGIO KWA VIGOGO>>>

Kaimu Rais wa Simba, Dokta Salim Abdallah alisema, baada ya kamati ya zabuni kumtangaza mshindi wa mchakato wa uwekezaji wa klabu hiyo, wajumbe watano wa kamati ya utendaji watapunguzwa na kubaki saba ambao wataingia kwenye bodi itakayoundwa.

WAJUMBE watano wa kamati ya utendaji ya Simba, watalazimika kukaa kando kupisha mabadiliko yatakayofanyika baada ya klabu hiyo kuingia katika mfumo wa hisa.

Kaimu Rais wa Simba, Dokta Salim Abdallah alisema, baada ya kamati ya zabuni kumtangaza mshindi wa mchakato wa uwekezaji wa klabu hiyo, wajumbe watano wa kamati ya utendaji watapunguzwa ili kubakia na saba ambao wataingia kwenye bodi itakayoundwa.

"Baada ya kamati ya zabuni kumtangaza mshindi, kamati ya utendaji itaanza kazi mara moja kutangaza wajumbe saba ambao wataungana na wajumbe saba upande wa mwekezaji, kuunda bodi ya kusimamia klabu yetu," alisema Abdallah.

"Wajumbe wa kamati ya utendaji wapo 12 ambao hawawezi kuingia wote kwenye bodi hivyo baadhi yetu hawatopata nafasi ya kuingia."

No comments:

Post a Comment