Vinara wa ligi kuu, Simba wataoandoka jijini Dar es Salaam kesho Alhamisi kwenda mkoani Mtwara tayari kuendelea na Ligi Kuu Bara dhidi ya timu ngumu ya Ndanda FC.
Simba inayoongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 23, jana jioni iliingia kambini baada ya kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Dar.
Jumamosi ijayo, Simba itapambana na Ndanda katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Meneja wa Simba, Richard Robert, amesema: “Timu imeingia kambini jana (Jumanne) kwa ajili ya maandalizi na kesho Alhamisi timu inatarajiwa kuondoka hapa Dar kwenda Mtwara na lengo ni kuhakikisha tunarejea na alama tatu,” alisema.
Simba msimu uliopita katika Uwanja wa Nangwanda ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, wafungaji wakiwa Mzamiru Yassin na Mohamed Ibrahim ‘Mo’.
No comments:
Post a Comment