Sakata la Airtel: TTCL Yamwaga Mboga
Muungwana Blog 2 · 42 minutes ago

IKIWA imepita siku moja tangu Rais John Magufuli amwagize Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, kuchunguza undani wa suala la umiliki wa kampuni ya simu ya Airtel, siri zaidi kuhusiana na kile kilichofanyika katika ‘dili’ za mauziano zimeanza kuanikwa.
Akizungumza mjini Dodoma juzi, Rais Magufuli alimtaka Dk. Mpango kuchunguza undani wa kampuni ya Airtel baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa kampuni hiyo inapaswa kuwa chini ya umiliki wa Kampuni ya Simu (TTCL), ambayo ni ya serikali. Pia Rais Magufuli alieleza wazi kuwa kuna ‘mchezo mchafu’ uliofanywa na baadhi ya watu katika suala hilo.
Kutokana na agizo hilo la Rais Magufuli, jana, TTCL, kupitia kwa mwenyekiti wake wa sasa wa bodi ya wakurugenzi, Omar Nundu, na Ofisa Mtendaji Mkuu, Waziri Kindamba, iliibuka na kuanika undani wa mambo kadhaa kuhusiana na kampuni hiyo, mojawapo ikiwa namna vigogo watano walivyoketi kwa siku moja na kufanya uamuzi unaoibua maswali mengi kwa sasa kuhusiana na umiliki wa kampuni ya Airtel. Kimahesabu, siku moja ina saa 24.
Alipoulizwa jana kuhusiana na suala hilo linaloambatana na madai kwamba TTCL ndiyo inayoimiliki Airtel Tanzania, Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Jackoson Mbando, alisema jambo hilo hawawezi kulizungumzia kama watendaji bali wamiliki wa hisa walio nje ya nchi ndio wenye wajibu huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Nundu alisema chanzo cha yote kilianzia Agosti 5, 2005, wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi za TTCL na Celtel wakati huo na wajumbe watano ambao majina yao hakuwa tayari kuyataja, walipokutana siku hiyo moja na kubariki uamuzi mzito uliofikisha jambo hilo lilipo sasa.
Nundu alisema bodi hiyo ilikuwa na watu tisa, lakini siku hiyo moja waliketi watano kati yao na kufanya uamuzi huo mazito huku wakiongozwa na mwenyekiti ambaye wakati huo alikuwa amekabidhiwa asilimia moja ya hisa zilizokuwa zikimilikiwa na ‘mtu asiyejulikana’.
Nundu alisema Celnet ilianzishwa na TTCL Mei 7, 2001 kwa mtaji wa Sh. bilioni moja na thamani ya hisa ikiwa Sh. milioni moja.
Alibainisha kuwa TTCL ilikuwa ikimiliki hisa moja huku thamani ya hisa ilikuwa Sh. 1,000 na mtu asiyejulikana alikuwa akimiliki hisa moja yenye thamani pia ya Sh. 1,000, kuanza baishara kwa jina la Celtel.
Hata hivyo, Nundu alisema hisa moja ya mtu asiyejulikana ikashikiliwa na raia wa kigeni na kwamba baadaye, TTCL ilitoa bilioni tano kwa ajili ya mtaji ili kampuni ianze kufanya kazi.
"Ilianzishwa kampuni inaitwa Celnet…imeanzishwa na TTCL,…ikapewa masafa megawati 900. Ilipofika wakati wa kufanya kazi, ikabadilishwa na kuwa Celtel, kampuni hii ilianzishwa na TTCL Mei 7, 2007 mtaji wake ukiwa Sh. bilioni moja, maana yake hisa milioni moja na kila hisa ina thamani Sh. 1,000,” alisema Nundu.
“Lakini wanahisa wakawa wawili, TTCL yenyewe ikachukua hisa moja, mtu asiyejulikana akachukua hisa moja, lakini akaishika raia wa kigeni. Kwa maana hiyo, kampuni ikaanzishwa kwa fedha Sh. 2,000," alisema Nundu.
Aidha, Nundu alisema TTCL ilitoa pia fedha zaidi ya Sh. bilioni 82 kwa ajili ya biashara huku cha kushangaza, mtu asiyejulikana akiwa hajatoa kitu chochote.
"Kama si TTCL kutoa Sh. bilioni tano, hakuna ambacho kingefanyika. Hakukuwa na uhitaji wa mwekezaji…. isitoshe TTCL iliweka Sh. bilioni 82 na ushee kuikopesha Celtel…sasa hapo unaona ni kampuni ya TTCL," alisema Nundu.
Alisema baadaye, raia wa kigeni aliyekuwa akishikilia hisa moja ya mtu asiyejulikana aliikabidhi kwa Mtanzania ambaye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL na pia Celtel.
“Siku ya kikao hicho, mwenyekiti wa bodi (ambaye ndiye aliyekabidhiwa hisa hiyo moja ya mtu asiyejulikana) na wajumbe wengine watano walifanya maamuzi (uamuzi) magumu (mgumu) ya kuirudisha hisa hiyo moja na kuikabidhi TTCL, hivyo TTCL ikawa inamiliki Celtel kwa hisa zote kwa asilimia 100,” alisema.
Akieleza zaidi kuhusiana na ‘mchezo’ uliofanyika, Nundu alisema thamani ya hisa asilimia 100 za TTCL ilikuwa Sh. bilioni moja, lakini wakakubaliana siku hiyo kuo

No comments:
Post a Comment