KENYA WATUMIA VYEMA UWANJA WA NYUMBANI , BURUNDI WASEMA HAIKUWA BAHATI>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Thursday, December 14, 2017

KENYA WATUMIA VYEMA UWANJA WA NYUMBANI , BURUNDI WASEMA HAIKUWA BAHATI>>

Wenyeji wa mashindano ya CECAFA Chalenji Cup,Kenya wametingafainali ya mashindano hayo baada ya kuifunga Burundi kwa  bao 1-0 katika dakika 120.

Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya 0-0, bao la Kenya lilifungwa na kiungo wa AFC Leopards,Wyvonne  Isuza Kinayangi dakika ya 100.

Mchezo mwingine wa nusu fainali ya pili, utachezwa kesho kwenye uwanja wa Moi mjini Kisumu kati ya wawakilishi walio salia wa Tanzania,Zanzibar dhidi ya Uganda.

Mshindi wa nusu fainali hiyo ya pili ataungana na Kenya kucheza mchezo wa fainali utakaochezwa Jumapili huku kukitanguliwa na mchezo wa mshindi wa tatu kwa timu zilizopoteza mechinusu fainali.


No comments:

Post a Comment