Uongozi wa Simba umemalizana na mlinzi wake wa kati raia wa Uganda Juuko Morshidi na amekubali kusaini mkataba mpya kuendelea kuitumikia Simba.
Aidha kiungo Mzamiru Yassini anatarajiwa kusaini mkataba mpya baada ya kurejea nchini kutokea Kenya anakoshiriki michuano ya Chalenji na Kilimanjaro Stars.
Mikataba ya Juuko na Mzamiru imebakisha chini ya miezi sita na walikuwa wakinyemelewa na klabu ya Yanga.
Wakati huo huo taarifa zimebainisha kuwa enchi la ufundi la Simba limeridhishwa na kiwango cha mshambuliaji raia wa Zambia Jonas Sekuhawa ambaye yuko nchini kufanya majaribio.
Sekuhawa alifunga moja ya mabao ya Simba kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Mchezaji huyo huenda akasajiliwa na hivyo kuweka mashakani hatma ya wachezaji wa Kimataifa, Laudirt Mavugo na Methodi Mwanjali.

No comments:
Post a Comment