Kocha mkuu wa Simba, Joseph Omog ameamua kukatisha mapumziko yake ya wiki moja na kwenda nchini Kenya kwa ajili ya kufatilia kiwango cha mshambuliaji Elias Maguli ambaye pia anawindwa na miamba mingine ya soka nchini Yanga.
Omog ameiambia Goal, akiwa kwao Cameroon alikokwenda siku nne zilizopita kuwa anamuhitaji mshambuliaji huyo kwa ajili ya kuimarisha safu yake ya ushambuliaji ambayo imeonyesha mapungufu katika mechi 11, za ligi alizocheza hadi sasa.
“Nataka kwenda Kenya lakini haitakuwa kwa ajili ya Maguri peke yake bali hata wachezaji wengine kwasababu pale kuna mataifa tisa yanashiriki michuano ya CECAFA Chalenji hivyo nisehemu nzuri ambayo inaweza kutusaidia kupata wachezaji wazuri,”amesema Omog.
Katika ripoti yake ya mapendekezo ya usajili Omog, alipendekeza kuongeza wachezaji wanne katika nafasi zote ikiwemo kipa beki wa kati na pembeni kiungo mmoja na mshambuliaji akidai kuwa nafasi hizo ndiyo zilizoonyesha mapungufu katika mzunguko huu wa kwanza.
Simba inamuhitaji Maguri, baada ya kupita misimu miwili ilipomtema kwa madai hana kiwango cha kuichezea timu hiyo na ndipo mchezaji huyo akaamua kwenda kucheza soka Stand United baadaye Oman huko Ugaibuni.
Karibu
No comments:
Post a Comment