AMKENI MAWAKALA JUU YA VIPAJI HIVI
Yahya Zayd
Huyu ni mshambuliaji kinda wa Azam FC, ni mmoja wa wachezaji chipukizi walioanza kucheza ligi kuu Tanzania bara msimu huu. Ana uwezo mzuri kucheka na nyavu pia kuchezesha wenzie. Ni wakati sahihi kwa sasa mawakala kumtazama kwa jicho la tatu kwa ajili ya kumtafutia timu nje.
Ramadhani Kabwili
Golikipa namba tatu Yanga SC, ni zao la Azam FC na ameendelea kuaminika na mabingwa hao wa ligi na timu ya taifa . Kuna kipaji kikubwa ndani yake endapo mawakala watamtafutia timu nje katika umri huu mdogo anaweza kuwa msaada kwa taifa kwa muda mrefu.
Mohamedi Issa ' Mo Banka '
Kiungo mshambuliaji Mtibwa Sugar! ananyemelea na Yanga dirisha dogo la usajili. Ni moja ya wachezaji wenye umri mdogo na kipaji maridhawa . Tusisubiri umri usogee ndio tumtafutie timu . Wakati ni huu ! Trial kadhaa nje zitamjenga zaidi kisoka na kumpatia vitu vipya .
Ramadhani Kichuya
Ni injini ya Simba SC wing ya kulia kwa sasa! Ni msimu wa pili sasa na mabingwa hao wa kombe la ASFC lakini ameendelea kuonesha uwezo mkubwa . Kikubwa ndani yake mbali na kipaji ni nidhamu ndani ya uwanja na nje ya uwanja. Anahitaji changamoto mpya nje!
Eliud Ambokile
Mshambuliaji Mbeya City FC mpaka sasa ana goli 4 ukiwa msimu wake wa kwanza ligi kuu baada ya kupandishwa toka timu B!. Ni kijana mdogo na mwenye uwezo mzuri kucheka na nyavu pia kusimamia mfumo wa kushambulia wa timu . Ni wakati wake huu wa mawakala kumtazama na kumpeleka nje . Uwezo wa kupeleka vijana katika umri mdogo ndio kitu sahihi katika mizani ya soka la kulipwa.
Ibrahim Ajibu
Amekuwa mpya ndani ya Yanga SC ! si Ibrahim yule aliyekuwa analalamikiwa kwa uvivu . Ana nguvu, kasi na uwezo mzuri wa kufunga na kuchezesha timu kama playmaker. Ni wakati sasa wa mawakala na klabu yake kumtafutia timu nje ili kuendeleza kipaji chake , klabu kuvuna pesa na nchi kufaidi matunda ya kipaji chake timu ya taifa .
Mzamiru Yassin
Injini ya Simba SC eneo la kati . Ni kiungo mwenye uwezo mkubwa kusimamia mifumo yote miwili ya timu kwa wakati mmoja ; kusimama kama kiungo mkabaji na mchezeshaji wa timu lakini pia ana uwezo mzuri wa kufunga . Ni msimu wake wa pili na Simba lakini bado anadhihirisha ubora wake. Ni wakati wake sasa kumtagutia soko nje!.
Himidi Mao
Wakati ukuta ! ni mmoja ya viungo waliodumu au kucheza mechi nyingi za klabu yake ya Azam na timu ya taifa kwa sasa ! Himidi hahitajiki kuingia katika orodha ya wachezaji wa kitanzania ambao hawakuweza kulivusha soka lao nje ya mipaka ya nchi kwa kipaji alichonacho.
Andrew Vincent ' Dante '
Ameanza kusimama kama muhimili wa Yanga SC eneo la ulinzi. Uwezo wake umemfanya kuipangua pacha ya muda mrefu katika eneo hilo , Nadir Haroub na Kelvin Yondani. Amerithi vyema mikoba ya Nadir na akiongeza umakini hakika ni dhahiri anakwenda kuwa tegemeo timu ya taifa na klabu yake . Ni wakati sasa wa mawakala kumtazama kwa soka la kulipwa nje !
Salumu Kipaga
Mlinzi wa kati Singida United. Katika mechi yao dhidi ya Yanga SC jumamosi iliyopita , alisimama vyema kuwazuia washambuliaji mahiri wa Yanga wasiweze kupata nafasi ya kufunga . Uwezo wa kupambana na Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa ulionesha kipaji chake kilivyo kikubwa kuweza kucheza sehemu yoyote duniani.
Aishi Manula
Tanzania One. Ni dhahiri kwa sasa ndie mlinda mlango bora mzawa nchini mwenye uwezo mkubwa wa kulilinda vyema lango lake . Ana tuzo ya kipa bora mara mbili mfululizo nchini ligi kuu Tanzania bara . Ni nadra sana makipa nchini mwetu kutoka nje ya nchi lakini kwa uwezo wake kama atapata fursa kuna uwezekano wa kufanikiwa katika hilo.
Rashidi Mandawa
Huyu ni mshambuliaji wa Tanzania Prisons akiwa na goli 6 kibindoni hivi sasa tofauti ya goli 8 na kinara wa orodha hiyo Emanuel Okwi. Si mara ya kwanza Mandawa kuingia katika orodha ya wafungaji wa ligi akiwa na zaidi ya goli 3! . Ni mshambuliaji mwenye uwezo mzuri kucheka na nyavu . Endapo atapata timu nzuri nje yenye viungo wazuri kumtengenezea nafasi ni dhahiri atacheka sana na nyavu!.

No comments:
Post a Comment