AJIBU NA CHIRWA KULETEWA WAPINZANI WAO DILISHA DOGO, WAO WASEMA WAKOFITI KUPIGANIA NAMBA>>>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Wednesday, November 8, 2017

AJIBU NA CHIRWA KULETEWA WAPINZANI WAO DILISHA DOGO, WAO WASEMA WAKOFITI KUPIGANIA NAMBA>>>>

YANGA WASIFANYE MAKOSA KIPINDI CHA DIRISHA DOGO LA MSIMU HUU.

Ni kipindi kingine tena ambapo timu za ligi kuu zina takiwa kufanya usajili unaolenga kuziba mapungufu yaliyojitokeza kwa mechi hizi za ligi hasa mwanzoni mwa msimu.Usajili huo wa dirisha dogo unatarajiwa kufunguliwa tar 15 Novembe mwaka huu.Hapa timu zinapaswa ziwe serious kidogo hasa wale ambao wanahusika na masuala ya Usajili (Kamati za Usajili).

Yanga ambao wana jukumu la kuiwakilisha nchi katika mashindano ya klabu bingwa barani Africa, wanapaswa watumie fursa hii kutengeneza kikosi imara ambacho kinaweza kupambana kimataifa zaidi.

Ni muda mahususi sasa kwa George Lwandamina kwenda kuonana na kamati ya Bwana Hussein Nyika ambae alifanya kazi kubwa sana kabla msimu kuanza katika kipindi cha usajili.Mwalimu anatakiwa apeleke mapendekezo ya wachezaji atakao wahitaji kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake.Halafu itakuwa kazi ya Nyika kuanza shughuli yake mara moja.

~…Haya ni baadhi ya maeneo muhimu ya kufanyiwa kazi:-

  1.CENTRAL BACK.
Yanga bado wana tatizo katika eneo la beki wa kati.It's obvious kwamba baada ya kuondoka kwa Mtogo Vicent Bossou bado hata patikana beki ambae angeweza kusimama na beki wa mwisho (Kevin/Nadir) akacheza kama sweeper.Huyu atakuwa na kazi ya kwenda kufanya clearance ya mipira yote inayopigwa kuelekea kwenye zone yao.Dante Vicent amejitaidi sana lakini bado anakosa ule umakini.Sio beki wa kutulia akafanya majukumu yake na kumsaidia Kevin.Anatakiwa beki mwenye kariba ya Abdi Banda wa Baroka ambae anakwepo kwenye nafasi na kwa muda sahihi.Thus why hata National Team Kevin akicheza na Banda huwa anatulia sana.

 2.VIUNGO WA PEMBENI.
Baada ya kuondoka Msuva ambae alikuwa na nguvu kubwa ya kuamsha mashambulizi akitokea kulia,Yanga wamehangaika vilivyo but sifa zimuendee mwalimu kwa kuangalia mbinu mbadala ya kumtumia Buswita  japo haja deliver kile alichokwa aki deliver Msuva.Ni fursa sasa afanye usajili wa winga mmoja wa kulia ikibidi hata wawili ambao wanaweza kutumia miguu yote miwili kama alivyo Kichuya.
Ningepata nafari ningemnong'oneza George amsajili yule Salum Kabunda wa mwadui fc.Kijana matata sana yule.Ana sifa zote za kuitumikia Yanga kwa sasa.

 3.ENEO LA MWISHO.
Wanatakiwa washambuliaji kama wawili ambao wana uwezo wa kucheka na nyavu.Yaani wale ambao ni wapambanaji tena wana macho ya mpira.Hao watawakuta Ajib na Chirwa pale.

~.......Ngojeni ninywe maji kwanza

No comments:

Post a Comment