TAYARI NDEMLA YUPO SWEDEN,HIVI UNAFIKIRI MAFANIKIO NI KITU RAHISI? HIZI NDIO NJIA ALIZOPITIA
SAID HAMISI NDEMLA
Date of birth: Mar 11, 1996
Age: 21
Nationality: Tanzania
Position: Midfield
Current club: Simba SC
KLABU ANAYOIPENDA:CHELSEA
Kuhusu wazazi wake na soka, Ndemla anasema baba yake, Khamis Ndemla (marehemu) na mama yake, Brandina Mwingira wamempa baraka zote katika ajira yake hiyo.
MAISHA NJE YA SOKA
Ndemla anasema anapokuwa hana majukumu na soka anapenda kutulia nyumbani na kusikiliza muziki.
Ndemla anaenda mbali na kuzungumzia chakula anachokipenda, anasema: “Nafurahi zaidi ninapopata ugali, samaki, maharagwe na mchicha kidogo, hapo safi kabisa.”
HISTORIA
Ndemla ni mtoto wa pili kuzaliwa katika familia ya watoto wanne. Ndugu zake wengine ni dada yake, Mwazani na wadogo zake wanaume ambao ni Ramadhani na Hamza. Ndemla alisoma Shule ya Msingi Uzuri na alimaliza elimu ya sekondari katika Shule ya Makongo, zote za Dar es Salaam.
Anasema alianza kujifunza soka katika akademia ya Soka Rangers chini ya kocha, Ramadhani Kipira. Timu hiyo ndiyo iliyomkuza na kwa sasa ipo chini ya kocha mwingine.
Anasema baada ya hapo alichukuliwa na Klabu ya Mesina ya Magomeni na kushiriki mashindano mbalimbali ya vikombe vidogo likiwamo Kombe la Kinesi.
*ALIVYOTUA SIMBA*
“Tulikuwa kwenye mashindano ya Kinesi kama kawaida, mimi nikiwa na klabu yangu ya Red Cross, hapo tukacheza na Simba B, tuliwafunga mabao 2-0, mimi nilicheza kama kiungo na ndiye nilifunga mabao yote, ndipo viongozi wa Simba waliniona na kunipenda.
Walichukua namba yangu ya simu na baadaye usiku walinipigia na kunitaka nijiunge Simba,” anasema Ndemla.
Akiwa Simba B wamechukua vikombe mbalimbali kama Uhai, Super 8 na
Kinesi, pia alishiriki mashindano magumu kama Kombe la Mapinduzi.

No comments:
Post a Comment