YANGA MAZOEZINI KUIWINDA STAND UNITED , SIMBA KAMA KAWA KILELENI>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Sunday, March 11, 2018

YANGA MAZOEZINI KUIWINDA STAND UNITED , SIMBA KAMA KAWA KILELENI>>

Kikosi cha Yanga kitafanya mazoezi ya mwisho Jumapili ya leo kabla ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stand United.

Yanga itashuka Uwanja wa Taifa kesho ikiwa na utofauti wa alama tatu pekee kuwa sawa na Simba anayeongoza ligi hivi sasa.

Mchezo huo utakuwa wa mwisho kwenye ligi, kabla ya safari kuelekea Gaborone kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Township Rollers FC.

Katika mchezo wa ligi uliopita, Yanga iliipa kichapo kikali Kagera Sugar cha mabao matatu kwa sifuri.

No comments:

Post a Comment