RASMI HAJI MANALA AIKIMBIA MANCHESTER UNITED , MASHABIKI SIMBA WAINGIWA NA HOFU KWA UDHAIFU ALOUONESHA>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Wednesday, March 14, 2018

RASMI HAJI MANALA AIKIMBIA MANCHESTER UNITED , MASHABIKI SIMBA WAINGIWA NA HOFU KWA UDHAIFU ALOUONESHA>>


Kufuatia kipigo cha mabao 2-1 ilichokipata Manchester United kutoka kwa Sevilla kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Sevilla, Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, ameamua kuacha kuishabikia timu hiyo.

United imeondolewa kwenye mashindani hayo baada ya kukubali kichapo cha mabao hayo, ikiwa ni hatua ya 16 bora ya mashindano.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika kuwa sasa atabaki kuishabikia Real Madrid na nyota wake Cristiano Ronaldo.

Mbali na kuachana na United, Manara pia ameeleza kuwa Jose Mourinho ni Kocha wa hovyo kuliko wote duniani kwa sasa, huku akisema atarudi kuishabikia tena timu hiyo pale Mourinho atakapoondoka.


No comments:

Post a Comment