Kocha wa Simba, Irambona Masoud Djuma amesema kikosi chake kilicheza vizuri lakini hakikufanikiwa kufunga.
Djuma raia wa Burundi amesema kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam FC ni sehemu ya kile ambacho wanajifunza na lazima watakifanyia kazi.
Kocha huyo amesema: “Tulicheza vizuri na tulistahili kushinda, lakini hatukufanya hivyo na hii ni sehemu ya mafunzo ya mpira.
“Nafasi ya kuyafanyia kazi matatizo yetu yatakuwa dhidi ya URA, haitakuwa mechi rahisi. Watuunge mkono na sisi tutapambana uwanjani kurekebisha.”
Simba ilipokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam FC katika mechi ya Kombe la Mapinduzi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, jana.
No comments:
Post a Comment