KILA LA HERI DONALD DOMBO NGOMA KWAHERI YA KUONANA>>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Tuesday, November 28, 2017

KILA LA HERI DONALD DOMBO NGOMA KWAHERI YA KUONANA>>>

Ngoma aitosa Yanga rasmi

MONDAY NOVEMBER 28 2017
     



In Summary
Mshambuliaji huyo tangu kuanza kwa msimu huu amekuwa akisumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara

ADVERTISEMENT
Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma ameitwaa katika kikosi cha Zimbabwe kitakachoshiriki mashindano ya Kombe la Chalenji kama mchezaji huru.

Kocha wa Zimbabwe, Sunday “Mhofu” Chidzambwa ametangaza kikosi cha wachezaji 29 watakaoingia kambini kesho kujiandaa na Chalenji akiwamo Ngoma.

Katika wachezaji 29, Ngoma aliyeondoka Yanga akiwa majeruhi ametajwa katika safu ya ushambuliaji pamoja na Dominic Chungwa (CAPS United), Clive Augusto (Ngezi Platinum), na Terrence Dzvukamanja (Ngezi Platinum).

Hivi karibuni taarifa za kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zinasema klabu hiyo ilitoa muda maalum kwa Ngoma aliyetimkia kwao Zimbabwe endapo atashindwa kurejea Dar es Salaam hadi Ijumaa saa sita usiku atasimamishwa.

Mbali na kusimamishwa Ngoma endapo atashindwa kuheshimu muda huo kesi yake itapelekwa katika kamati ya nidhamu ya klabu hiyo ambapo uamuzi ya kumtimua kabisa yanaweza kuchukuliwa.

Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amethibitisha mshambuliaji wake huyo amepewa muda wa kuhakikisha anakuja nchini kujieleza kwa utoro wake.

"Nimeambiwa na uongozi kuwa alitakiwa (Ngoma) kuwa nchini Novemba 24 sasa kama hatakuja au atakuja hayo yataamuliwa na uongozi," alisema Lwandamina.

Hata hivyo kikosi hicho cha Zimbabwe kinategemea kupunguzwa na kubaki 20 kabla ya kwenda Nairobi, Kenya mwishoni mwa wiki tayari kwa mashindano hayo.

Kikosi cha Zimbabwe: Makipa: Takabva Mawaya (Ngezi Platinum), Elvis Chipezeze (Chicken Inn), Herbert Rusawo (Black Rhinos).

Mabeki: Devine Lunga (Chicken Inn), Praise Tonha (How Mine), Qadr Amini, Partson Jaure (Ngezi Platinum), Farai Madhananga (Harare City), Peter Muduviwa (Highlanders), Jimmy Dzingai (Yadah), Collen Kwaramba (Chapungu), Kelvin Moyo (FC Platinum), Stephen Makatuka (CAPS United).

Viungo: Devon Chafa (CAPS United), Gerald Takwara (FC Platinum), Never Tigere (ZPC Kariba), Liberty Chakoroma (Ngezi Platinum), Rodwell Chinyegetere (FC Platinum), Ishmael Wadi (Bulawayo City), Raphael Manuvire (ZPC Kariba), Ocean Mushure (Dynamos), Ali Sadiki (FC Platinum), Clement Matawu (Chicken Inn), Martin Vengesayi (Harare City).

Washambuliaji: Dominic Chungwa (CAPS United), Clive Augusto (Ngezi Platinum), Terrence Dzvukamanja (Ngezi Platinum), Donald Ngoma (huru).

Benchi la ufundi: Sunday Chidzambwa (kocha), Rahman Gumbo (kocha msaidizi), Lloyd Mutasa (kocha msaidizi), Brenna Msisika (kocha wa makipa), Patrick Mutesva (meneja wa timu), Shakespeare Chinogwenya (tunza vifaa), Somani Mudariki (daktari), Thompson Matenda (daktari wa viungo

No comments:

Post a Comment